Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Kwanza kabisa kuvamia Marekani Iran ni ndoto za wendawazimu kwa kua kauli hiyo si ya kwanza kutamkwa na Marekani na kila siku hujitahidi kusambaza propaganda hiyo ulimwenguni.
Marekani kuvamia Iran ya baki kua ni maneno ya kisiasa tu na kupiga chenga watu wasiojua Iran ni nchi gani.
Tunaposema kua Marekani hawezi kuvamia Iran ni kutokana nukta hizi zifuatazo:
1- Utakapo kua mfuatiliaji wa habari ni kua kila nchi inayopakana na Iran kuna kambi ya kijeshi ya Marekani kama Azerbaijan, Uturuki, Afghanistan, Pakistan, Iraq na Bahrain, Kambi zote za kijeshi katika kila nchi hiyo ni maadalizi ya kuvamia Iran ila Marekani hadi sasa hajafaanisha suala hiyo kwa kua kila aina ya ujasusi aloutumia alifeli na Iran haraka sana alifahamika nini ataka kufanya, Kama ilivyokua mwaka wa mawindo wa ndege za kijasusi za Marekani katika anga la Iran, Jeshi la Iran baada ya kufaanikiwa kunasa ndege ya kijasusi ya Marekani RQ170 mwaka jana Jeshi la Majini la Jamuhuri ya Kiislam ya Iran lilinasa ndege nyengine ya kijasusi ya Marekani itwayo Scan Eagle NQ1 katika Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf).
Mara kadhaa ndege za kijasusi za Marekani zilikua zikikusanya ripoti tofauti katika anga ya Jamuhuri ya Kiislam ya Iran na kila zilipokua zikikaribia katika anga la Iran zilikua zikishambulia na Jeshi la Jamuhuri ya Kiislam ya Iran.
Ndege hiyo ilitengenezwa na Shirika Ndege la Bowing, Na ndege hiyo mwazo ilikuwa ikitumiwa katika kulinda Bahari na kudhibiti uvuvi haramu ila baada ya kupita miaka na kuzidishiwa teknolojia ndege hiyo ilianzwa kutumiwa na Jeshi la Majini la Marekani katika masuala ya kijasusi.
Ndege hiyo ilotengenezwa na Shirika la Bowing baada ya kuongezewa teknolojia ilitumiwa katika vita ya Iraq mwaka 2004 kudhibiti maeneo tofauti ya kivita nchini Iraq.
Kunaswa ndege hiyo Gazeti moja la Marekani liliuliza: Wabobezi wa Iran ni njia gani waloitumia kunasa Scan Eagle NQ1 baada RQ170?!
Gazeti hilo la Marekani liitwalo Cristian Science Monitor liliripoti: Kunaswa Scan Eagle NQ1 katika shereheza mwaka ilonaswa RQ170 ni pigo kubwa kwa Marekani na mshirika wake Israel.
Gazeti la Marekani Cristian Science Monitor lilinakili maneno ya Bw.Patrison ambae alipongeza Jamuhuri ya Kiislam ya Iran kuinasa RQ170 mwaka ulopita akisema: Kunaswa kwa mara nyengine tena ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya Scan Eagle NQ1 ni mafaanikio na kuonyesha kiasi gani Iran imeendelea kiteknolojia.
Akiendelea kusema: Teknolokia ilotumiwa kunaswa Scan Eagle NQ1 inaitwa UDANGANYIFU ambayo imetumiwa na wabobezi wa Iran kutumia GPS ndege hiyo, Teknolojia hii inatumiwa kuchanganya sistim ya ndege na kusikia ujumbe wa kuamrishwa kushuka na kudhani kua amri na ujumbe huo ni wa kutuo kikuu na kushuka katika mikono ya adui.
Akimalizia kwa kusema: Ila teknolojia hii hutmiwa pale tu unapokua unataarifa zaidi ya ndege, La ajabu ni kwamba Je! Iran ilikua na taarifa kamili ya Scan Eagle NQ1?! Na teknolojia hiyo nani kawafundisha? Hii ni ishara kua Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran imesonga mbele katika teknolojia ya kivita kiasi ya kwamba hakuna anaejua teknolojia yao imefikia wapi na hii ni hatari kwa kila nchi itayo thubutu kuivamia Iran hasa Marekani na Israel.
2- Marekani amiliki kambi kubwa mashariki ya kati makao yake makuu ni Bahrain na Bahrain ni moja kati ya nchi zilizopakana na Iran na hapo kabla Bahrain ilikua ni moja kati ya mikoa ya Iran, Kambi hiyo inazaidi ya miaka 26 ipo Bahrain kwa malengo ya kuvamia Iran, Na hatua hiyo ilichukuwa tu baada ya mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ila hesabu tangu mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hadi leo imepita miaka mingapi?! Utakapo kuwa mdadisi na mfuatiliaji wa siasa utatambua kua Marekani pamoja na kuwa moja kati ya nchi zenye nguvu duniani imeshindwa hadi sasa kuvamia Iran imebaki tu maneno ya kuivamia Iran ilihali ya kua kila pande imeizingira Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran na miongoni mwa kuivamia Afghanistan na Iraq ni kukamilisha opresheni zake za kuvamia Iran.
3- Vita ya Iran na Iraq ilodumu kwa muda wa miaka 8, Sababu ya vita hiyo kama ilivyoelezwa ni kudai Sadam Hussein kua Mkoa wa Ahwaz ni wa Iraq, Ila ukiangalia kiundani zaidi utakuta kua sababu sio hiyo bali ni kutaka kuangusha dola mpya ambayo ni Jamuhuri ya Kiislamu iloasisiwa na Imam Khomein, Yote ni kua mtawala wa kabla ya Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran alikuwa ni kibaraka wa Marekani na hiyo ilikua sababu kuu ya kuivamia Iran, Vita ilodumu miaka 8 alishuhudia mauaji ya kinyama na nchi nyingi zilishiriki katika vita hiyo kuipa silaha Iraq kwa ajili ya kuangusha dola ya Kiislamu, Miongoni mwa nchi hizo ni; Marekani, Ungereza, Saudia Arabia, Jordan, Kuwait, Qatar na Yemen.
Pamoja na kushiriki nchi nyingi katika vita hiyo hawakufaanikiwa kuingusha dola changa iloasisiwa na Imam Khomein sembuse leo hii Iran ni nambari moja mashariki ya kati kwa nguvu za kijeshi!.
4- Iran na Waislamu kiujula wamiliki imani iso tishiwa na kitu chochote kile ulimwenguni, Imani ya kua Muislamu anapofariki katika vita afa kishahidi wakimaanisha kuaga dunia na kuelekea ulimwengu mwengine, Tofauti na wasokua Waislamu hawana imani kama hii na hii ni fahari kwa Waislamu wote.
5- Maneno ya Imam Khomein, Miaka 30 ilipita takriban Imam Khomein alisema: Marekani hawezi kufanya chochote, Sisi twaiweka Marekani chini ya visigino vyetu.
Maneno haya ni ya miaka 32 ilopita na hadi sasa Marekani hajathubutu kuvamia Iran, Fikiria hivi kuna mtu au nchi yoyote ile ilishathubutu kukosoa Marekani au kutangazia ulimwengu kua lazima Israel ifutwe kwenye ramani ya dunia?! Hii ni Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran pekee ndio ya thubutu kusema kwa ujasiri maneno kama haya, Tumeshuhudia nini kilichoisibu Zimbabwe kufukuza wazungu na kunyanganywa mashamba yao!! Ila Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran haina kiziwizi chochote kile itakapo taka kukosoa mabeberu wa dunia wakiongozwa na Marekani.
Kwa mantiki hii uwezekano wa Marekani kuvamia Iran si rahisi kama wanavyosema kila siku katika vyombo vya habari, Kutokana na maelezo tuliotangulia kusema hapo awali kua Marekani ameizingira Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran na kama Marekani angelikua na nia ya kuivamia Iran siku nyingi angefanya hivyo ila vita dhidi ya Iran si maslahi ya Marekani kwani Jamuhuri ya Kiislamu sio ile nchi ya miaka 32 ilopita, Na hakuna nchi yaitambua Iran imefikia wapi kiteknolojia hadi sasa, Na hii ni hatari kwa kila nchi itayo thubutu kuivamia Iran hasa Marekani na Israel kulinga na madai yao.